Bondia Lulu Kayage (kushoto) akimrushia konde bondia Hamisi Berege wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwene Uwanja wa Msimbazi Rovers Ilala jijini |
MABONDIA wawili wa ngumi za kulipwa wanatarajia kuondoka
nchini kesho kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mapambano yatakayofanyika
Agosti 9, mwaka huu.
Akizungumza jijini kocha wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila
aliwataja mabondia hao kuwa ni Lulu Kayage na Ramadhan Shauri.
“Lulu na Shauri wamepata mapambano yatakayochezwa Agosti 9,
hivyo wataondoka kesho kwa ndege ya shirika la Ethiopia “, alisema Mhamila.
Pia Mhamila alisema Lulu atapigana na Lizbeth Sivhaga na
Ramadhan Shauri atapigana na bondia mzoefu Philip Ndlovu
Mapambano haya yatafanyika kwenye wa Limpopo hivyo watanzania
mnawaombwa kuwaombea mabondia hao ili waweze kupeperusha bendera ya taifa vema.
No comments:
Post a Comment