SHIRIKISHO la Mpira la Soka Tanzania
(TFF) limesaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara
msimu ujao na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa
amethibitisha kusainiwa kwa mkataba huo na kusema hawakufanya sherehe za kutia
saini mkataba huo kutokana na mashindano ya Kagame yaliyokuwa yanaendelea
nchini kwani TFF ndio iliyokuwa ikiyasimamia kama shirikisho la soka mwenyeji.
“Wanasema katika ajira,
unaposikia nafasi haijatangazwa na hajatangazwa mtu mpya basi kuna maendeleo na
mara nyingi mkataba unaoendelea uliokuwepo ukisainiwa tena ‘renewal contract’
haivuti masikioni kama unapoongelea mkataba ambao watu wameingia udhamini
mpya”, amesema Mwesigwa.
Pia Mwesigwa aliweka wazi kuwa mdhamini
wa ligi msimu unaokuja ni Vodacom ambao walikuwepo msimu uliopita kwani kila
kitu kimeshawekwa sawa ila kwa maana ya sherehe ndio bado haijafanyika
kwasababu kulikuwa na mambo mengi hapa katikati ikiwa ni pamoja na mashindano
ya Kagame.
Pamoja na kukiri kuwa TFF
imeshakubaliana na Vodacom kuendelea kwa miaka mitatu ijayo lakini hakuweka wazi
jinsi mkataba huo ulivyoboreshwa kwa madai hadi sherehe za kutiana saini
zitakapofanyika.
“Mkataba ni miaka mitatu, kutakuwa
na maongezeko ukizingatia kuna timu zimeongezeka lakini nadhani hata kile
kinachokwenda kwenye vilabu kitaongezeka kwa kiasi fulani yako masuala mengi
siwezi kuzungumza kwa undani kwa sasa hivi pia kwa upande wa kwetu tulikuwa na mambo ambayo tuliyaona hayapo sawa hivyo
kulikuwa na muda mwingi wa kutosha kujadili karibu miezi nane iliyopita kwa hiyo
vitu vingi vimeangaliwa”, alisema Mwesigwa.
Vodacom wamekuwa wakidhamini ligi
kuu lakini kumekuwepo malalamiko mengi kwa klabu kuwa kiasi wanachotoa hakitoshelezi
ukizingatia baadhi ya timu hazina mfadhili
No comments:
Post a Comment