WAZIRI ATEMBELEA MAZOEZI YA TIMU KUIPA MORALI IFANYE KWELI KWENYE MECHI YA KCCA LEO
Waziri wa Utamaduni, Vijana na Michezo wa Suadan Mh. Stephen Lado Onesimo akizungumza na wachezaji wa Malakia FC
Waziriwa wa Utamaduni, Vijana na
Michezo wa Sudani Kusini Mh. Stephen Lado Onesimo jana aliitembelea timu
ya Malakia FC wakati ikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume wakati
ikijiandaa kwa ajili ya mchezo wake wa leo dhidi ya KCCA ya Uganda
mchezo utakaopigwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Taifa
ikiwa ni mwendelezo wa mashindano ya Kagame Cup hatua ya makundi.
Waziri Stephen Onesimo akiwa nafatilia mazoezi ya Malakia kwenye uwanja wa Karume
Waziri huyo amesema, wachezi wa
Malakia wanahitaji kushinda mchezo huo japo tayari wananafasi ya kucheza
hatua ya robo fainali lakini ushindi kwenye mchezo huo utazidi
kuwajengea heshima kwenye soka la ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati
lakini pia watakuwa wanaweka heshima ya nchi yao (Sudan Kusini) ambayo
imekuwa ikibezwa kwenye soka tangu ijitenge kutoka Sudan (Kaskazini).
“Nidhamu kwenye mchezo ni kitu
muhimu sana, kila mtu anatakiwa awe na nidhamu ya hali ya juu wakati wa
mchezo, muelekezane wenyewe kwa wenyewe muwapo uwanjani nani anatakiwa
kufanya nini ili kumpunguzia kazi kocha wenu. Mimi nawatakia kila kheri
na ninaimani na ninyi na ninamatumaini tutashinda mbele ya KCCA”,
alimaliza.
Post a Comment