Taifa
Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager leo
jumamosi saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimba la
Nakivubo kucheza na wenyeji Uganda.(The Cranes).
Mecho
hiyo ya kesho ni mchez wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN
mwaka 2016 zitakazofanyika mapema mwezi Januari nchini Rwanda, mgeni
rasmi atakua Rais wa Uganda Yoweri Mseveni.
Kikosi
cha Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa, kiliwasili
jijini Kampala jana usiku na kimefikia katika hoteli ya Grand Global
iliyopo jirani na chuo kikuu cha Uganda Makerere.
Taifa
Stars imefanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Nakivubo yakiwa ni
mazoezi mepesi na mwisho kuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe
utakaofnayika kesho jioni.
Kocha
Mkwasa akiongelea kuelekea mchezo huo amesema, anashukuru vijana wake
wamefika salama wote, hali nzao ni nzuri, morali ni ya hali ya juu,
kikubwa wanatambua wana deni kubwa kwa watanzania hivyo kesho
watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Akiongelea
hali ya hewa na mazingira ya timu ilipofikia, Mkwasa amesema hali ya
hewa ni ya kawaida baridi na mvua kidogo haina tofauti sana na Tanzania,
mazingira ya hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki ni kusaka
ushindi katika mchezo huo na vijana wake wapo tayari.
Wakati
huo huo mashabiki zaidi ya 50 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa wamewasili alfajiri wakitokea jijini Dar es salaam kuungana
na watanzania wengine waishio nchini Uganda kuishangilia timu ya
Tanzania itakapokuwa ikipimbana na Uganda katika uwanja wa Nakivubo.
No comments:
Post a Comment