Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 1, 2015

PHIL JONES ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER UNITED.

Phil Jones, mwenye Miaka 23, amesaini Mkataba mpya na Man United ambao utambakiza Klabuni hapo hadi Juni 2019 pamoja na nyongeza ya Mwaka mmoja juu yake.
Jones alianza kuichezea Man United Mwaka 2011 na ameshacheza Mechi 128 na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara moja Mwaka 2013.
Akiongea baada ya kusainiwa Mkataba huo mpya, Meneja Louis van Gaal alisema: "Tumefurahi Phil amesaini Mkataba mpya. Yeye ni Mchezaji mwenye kipaji anaeweza kucheza nafasi nyingi. Bado ni Kijana anae endelea wakati wote."
Nae Phil Jones ameeleza: "Nimefurahishwa kusaini dili mpya. Hii ni Klabu kubwa kushiriki nayo na naungoja kwa hamu Msimu mpya."

No comments:

Post a Comment