Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 1, 2015

CECAFA YATOA RATIBA YA KAGAME 2015

Rais wa Vyama vya soka vya nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodgar Tenga (katikati) akifafanua jambo kuhusu mashindano ya CECAFA wakati wa mkutano na wandishi wa habari yatakayoanza Julai 18 jijini Dar es Salaam na kushirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama.Kushoto ni Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye na kulia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ambao ndio wenyeji wa mashindano, Jamal Malinzi. (Picha na Rahel Pallangyo)

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za TFF zilizopo Karume, Tenga ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.

Lengo la CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na kuahidi TFF itahakikisha michuano hiyo inafanya nchini katika hali ya amani na usalama toka mwanzo mpaka mwisho wa michuano hiyo.

Timu zilizothibtisha kushiriki michuano hiyo ni Yanga, Azam (Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA (Uganda).

Wakati huo Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.

Mechi ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya Somalia.


Ratiba ya michuano hiyo imeziweka timu hizo katika makundi matatu ambapo kundi A lina timu za: Yanga (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djbiout), KMKM (Zanzibar) na Khartoum-N (Sudan)

Kundi B: APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi) na Heegan FC (Somalia), Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda)

Timu tatu zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B & C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika hatua ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment