KLABU ya
Simba imezindua kadi mpya za uanachama ambazo zitatoa fursa kwa watakaojiunga kunufaika na bima ya
maisha.
Akizungumza leo kwenye uzinduzi huo Rais wa Simba Evans Aveva alisema kila mwanachama
atakayejiunga na kuchukua kadi mpya atapata bima ya maisha inayojulikana kama
Simba pamoja.
Alisema bima
hiyo ambayo hupatikana kwenye tovuti ya Simba itampatia mwanachama ambaye
amelipa malipo yake ya mwaka ya uanachama jumla ya Sh. 250,000 ikiwa atapata
msiba wa kwake, mwenza wake au mtoto.
Kwa mujibu
wa Aveva, malipo ya uanachama ni sh. 1000 kwa mweli hivyo ikiwa mwanachama
atalipa ada ya mwaka sh. 12,000 kwa
wanachama hai na sh. 30,000 kwa wanachama wapya ndipo atanufaika na bima hiyo
ya simba pamoja.
“Faida hii
ya huduma ya Simba pamoja itamwezesha mwanachama wa samba kupata mkono wa pole
apatapo msiba. Hii ndio klabu pekee Afrika Mashariki inayotoa fao hili kwa
wanachama, Simba inajali sana wanachama wake,”alisema.
Aveva pia,
alizindua kadi ya simba cubs kwa ajili ya watoto wanaoipenda timu hiyo ili
kuwawezesha kutambuliwa na kuwa wanachama wa timu hiyo.
“Kadi ya
Simba cubs itawawezesha watoto sio tu kutambuliwa kuwa mwanachama wa samba,
bali pia kupata punguzo kubwa au kuingia bure kwenye matukio yanayoandaliwa na
Simba na kwenye maduka yatatoa punguzo kwa watoto wenye kadi hizo,”alisema.
Ateua baraza la wazee
Katika hatua
nyingine Aveva alitangaza baraza la
wazee aliloliteua kwa ajili ya kuwashauri mambo mbalimbali ya klabu.
Baraza hilo
linaongozwa na Mwenyekiti Omary Mtika na wajumbe ni Ally Hassan, Abdulsharif
Zahoro, Chuma Suleiman na Omary Moshi.
Wakati huo
huo, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAG Group ambaye ni mwezeshaji wa klabu hiyo
Iman Kajuna alisema upatikanaji wa kadi hizo ni moja ya majukumu yao
waliyowekeana awali katika kuhakikisha wanabuni mbinu zitakazoisaidia klabu
hiyo kupata mapato.
Alisema
wanachana wanaohitaji kujiunga wanatakiwa kuomba maombi ya kupata kadi kupitia
tovuti ya klabu hiyo www.simbasport.co.tz
na kwamba kadi hizo zina uwezo wa kutunza kumbukumbu.
No comments:
Post a Comment