MSHAMBULIAJI mpya wa
Yanga Donald Ngoma, amewataka mashabiki wa timu hiyo kusubiri mambo
mazuri kutoka kwake ikiwa ni muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa miaka
miwili kuichezea timu hiyo
Ngoma aliyetambulishwa
rasmi leo kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga sambamba na beki Joseph
Zuttah, alisema amejipanga kufanya kazi kubwa na kuipa mafanikio timu hiyo ili
aweze kudumu kwa muda mrefu kama ilivyokuwa FC Platinum.
“Najisikia furaha
kucheza Yanga kwa sababu ni klabu kubwa Tanzania nitahakikisha natumia uwezo
wangu naipa naongeza mafanikio yaliyopo kwa kushirikiana na wenzangu nilio
wakuta,”alisema Ngoma
Kwaupande wake Zuttah
alisema ametua Yanga kwa kazi moja tu ya kuendeleza mazuri yaliyofanywa siku za
nyuma na amekuja akiwa kamili na kuwataka washabiki wa timu hiyo kumpa sapoti.
“Nimefurai kuona
mashabiki wanaipenda sana timu yao kuanzia Jumamosi wakati Yanga ilipocheza na
Sports Villa nimehamasika sana kitu ambacho kimenifanya nisijutie maamuzi yangu
ya kucheza Tanzania,”alisema Zuttah.
Kwa mujibu wa Mkuu wa
Habari wa Yanga Jerry Muro alisema wachezaji hao wameshamalizana nao kila kitu
na tayari wameshawasilisha usajili wao Shirikisho la soka Tanzania TFF, ili
waweze kuombewa kibali cha kufanyia kazi.
Ngoma ametua Yanga
akitokea FC Platinum ya nyumbani kwao Zimbabwe wakati Zuttah alikuwa akikipiga
klabu ya Medeama ambao
ni mabingwa wa Kombe la FA nchini kwao Ghana.
Baada ya kuwanasa
wachezaji hao wawili tayari Yanga imekamilisha idadi ya nyota saba wakimataifa
inayotakiwa na Kanuni za TFF nyota wengine wakimataifa ni Haruna
Niyonzima,Amissi Tambwe,Kpah Sherman,Andrey Coutinho na Mbuyu Twite.
No comments:
Post a Comment