UONGOZI wa
Simba umesema mchezaji wa zamani wa Yanga Hamis Kiiza atajiunga na klabu hiyo
kwenye mazoezi kati ya leo au kesho iwapo tu atafuzu vipimo vya afya.
Kiiza ambaye
alitemwa Yanga msimu uliopita alitarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia jana,
na leo atapimwa afya ili kuungana na wachezaji wengine wa Simba katika mazoezi.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari leo Rais
wa Simba Evans Aveva alisema Kiiza atakuwa mchezaji halali wa Simba iwapo
atafuzu vipimo leo.
“Kiiza
atatua muda wowote kuanzia leo na akifaulu vipimo vya afya moja kwa moja
atakuwa mchezaji wetu,”alisema.
Mchezaji
huyo Mganda alitemwa na aliyekuwa Kocha wa Yanga Marcio Maximo msimu uliopita
na nafasi yake kuchukuliwa na Kpah.
Kiiza hivi
karibuni alinukuliwa kwenye vyombo vya habari akithibitisha ujio wake wa
kujiunga na Simba.
Iwapo
atafanikiwa kusajiliwa Simba atatimiza jumla ya wachezaji wanne wanaotoka Uganda baada ya Emmanuel Okwi na
Simon Sserunkuma na Juuko Murshid huku Raphael
Kiongera akitokea Kenya.
No comments:
Post a Comment