Kiungo
Myarwanda, Jen Baptiste Mugiraneza, ameanza mazoezi na klabu ya mpya ya Azam
FC, leo.
Migiraneza maarufu kama Migi ameanza mazoezi na
kikosi cha Azam FC chini ya Kocha Stewart Hall kwenye Uwanja wa Chamazi jijini
Dar es Salaam.
Hata hivyo,
taarifa zimeeleza, Migi bado hajamalizana na Azam FC katika suala la mkataba na
huenda likafanyika leo mchana au jioni.
Kiungo huyo
nyota wa APR, pia ni tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda,
Amavubi.
No comments:
Post a Comment