Timu ya Taifa ya Tanzania ya
Wanawake kwenye umri chini ya miaka 20 (Tanzanite) kesho siku ya jumamosi
itashuka dimbani uwanja wa Azam Complex kucheza na timu ya Taifa ya Zambia
chini ya miaka 20 (Young She-Polopolo).
Viingilio vya mchezo wa
kesho kati ya Tanzanite dhidi ya Young She-Polopolo ni shilingi elfu mbili
(2,000/=) kwa jukwaa la mzunguko, na shilingi
elfu tatu (3,000/=) kwa Jukwaa Kuu.
Mchezo huo wa kuwania kufuzu
kwa Fainali za Wanawake za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Papua
New Guinea, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Sudan,unatarajiwa kuanza saa
10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na kati.
Timu ya Young She-Polopolo
tayari imeshwasili nchini jana jioni, na leo wakitarajiwa kufanya mazoezi
mepesi leo jioni katika uwanja wa Azam Complex kw ajaili ya mchezo huo. Waamuzi
wa mchezo huo kutoka nchini Sudan tayari wameshawasili.
Wakati huo huo Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetoa usafiri wa mabus mawili kwa ajili ya
kikundi cha ushangiliaji cha timu za Taifa (Taifa Supporters) kitachokwenda
kesho Chamazi kuipa sapoti timu ya Tanzanite.
Mabasi hayo mawili
yataondoka ofisi za TFF zilizopo Karume saa 6 kamili mchana kuelekea Chamazi
kwa ajili ya kuishangilia timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite).
No comments:
Post a Comment