Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 31, 2015

Maradona amtuhumu mkewe kumuibia fedha

Diego Maradona aibiwa fedha
Nguli wa soka Duniani ,Diego Maradona amemtuhumu mke wake wa zamani Claudia Villafañe kwamba kumuibia kiasi cha fedha zipatazo dola milioni tisa, katika akaunti yake ya benki.
Akizungumza katika matangazo ya moja kwa moja ya Luninga,Maradonna amesema Villafañe ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani ni mwizi. Hata hivyo Villafañe amepinga vikali madai na kudai kuwa yeye si mwizi na hakuiba fedha hizo.
Wapenzi hao ambao walikutana katika mji uliokithiri kwa umasikini huko Buenos Aires kabla ya Maradonna kuwa maarufu na kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri duniani katika historia ya soka,waliachana kimapenzi kutokana na kutofautiana.
Watoto wao wawili Dalma and Giannina,wamekaririwa kwenye mtandao wa twitter wakimtetea mama yao wazi wazi na kwamba hahusiki na upotevu huo wa fedha za baba yao.

No comments:

Post a Comment