Zikiwa
zimesalia siku chache kuanza kutimua vumbi kwa michuano ya Ligi kuu ya
Uingereza, mabingwa wa ligi hiyo timu ya Chelsea inatarajia kuivaa
Arsenal katika Mechi ya ufunguzi inayotambulika kama ngao ya jamii
itakayopigwa siku ya jumapili katika uwanja wa Wembley jijini London.
Ligi
hiyo inatarajia kuanza Augosti nane kwa michezo sita ambapo Manchester
United itachuana na Tottenham katika uwanja wao wa nyumbani wa Old
Trafford wakati Bournemouth watawakabili Aston Villa,Norwich city
wakipepetana na Crystal palace ,Leicester city ,nyumbani king power
kukipiga na Sunderland,Everton watachuana na Watford na Chelsea dhidi ya
Swansea city.
No comments:
Post a Comment