Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 31, 2015

Fukwe za Rio de Janeiro ni chafu.

Maeneo ya Fukwe za Rio De Jeneiro yatakako fanyika mashindano ya Olympik mwakani
Rais wa Kamati kuu ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach, amesema kuwa uchafuzi wa bahari ni moja ya kikwazo Rio de Janeiro katika maandalizi ya michuano ya hapo mwakani.
Hata hivyo kutokana na hali hiyo waandaji wa mashindano hayo ya riadha wamesema kuwa watafanya kila linalowezekana kwa afya ya wanariadha wakati wa Olympiki.
Takribani asilimia 70 ya maji taka yanamwagika Rio de Janeiro katika fukwe za Guanabara,eneo ambalo wapiga mbizi watafanyia mashindano yao.
Katika hali inayoonyesha ni hatari kwa afya wanariadha walioko kwenye mafunzo katika pwani hiyo wameona mizoga ya wanyama na uchafu ukiwa ukingoni mwa eneo hilo ambalo mashindano hayo yatafanyika.

No comments:

Post a Comment