MSANIIwa Bongo
Fleva, Khadija Shabani Taya au Keishaameibuka mshindi kwenye kura za maoni za Ubunge wa Viti Maalum kundi la
Walemavu mkoa wa Dodoma na kuwa mshindi wa kwanza.
Keisha
amepata kura 340 huku Stella Fueda akimfuatia kwa kupata kura 112, Anna Fungo
kura 100 na Graceana Kavishe kura 54.
Jumla
ya kura 721 zilipigwa, ambapo kura 75 ziliharibika na kura za halali zilikuwa
646.
Msanii
huyo aliwahi kuhojiwa na vyombo vya habari na kubainisha kuwa, japo ni mlemavu
wa ngozi lakini anajikubali, anajipenda, kujiamini na amekuwa akipigania amani
ambayo wanastahili kuipata kutoka nchini.
Alisemaalipoanza kuweka picha zake za siasa kwenye
mtandao kuna baadhi ya watu walimpongeza na wapo waliosema kuwa hana uchungu na
wenzake kwani waliamini anaingia kwenye siasa kwa nia ya kujinufaisha.
“Wapo
wanaohisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi ni mpiganaji
na ndio maana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu,” alisema.
Alisema
fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunjichawa akimaanisha kuwa lazima kusimamia
sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani, hivyo basi lazima kuwe na
wawakilishi wa kutosha ndani ya Bunge na sauti zisikike ili sheria kutungwa na
kutekelezwa pia.
Hiyoni hatua ya kwanza ya mchakato wa kusaka
nafasi ya kuwakilisha walemavu, ambapo sasa ataenda katika inayofuata ambayo
itahusishwa washindi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
STEVE BARKER NDIYE KOCHA MPYA SIMBA SC
-
KLABU ya Simba SC imemtambulisha Steven Robert ‘Steve’ Barker (57) kuwa
Kocha wake mpya Mkuu akichukua nafasi ya Mbulgaria, Dimitar Nikolaev Pantev
aliye...
Stronger Together. Ready for 2026.
-
*@Pictures by Mobila Safaris Team-Serengeti.*
*Stronger Together. Ready for 2026.*
Dear Partner,
As 2025 draws to a close, we want to thank you for...
Post a Comment