WAKALA wa kiungo Yaya Toure amedai kuwa ana uhakika wa asilimia tisini
kuwa mteja wake huyo ataondoka katika majira ya kiangazi. Aprili, Toure
ambaye amebakisha mkataba wa miaka miwili ambao unamuingizia kitita cha
euro 265,000 kwa wiki, alikuwa akitaka kufanya mazungumzo na maofisa wa
City kuhusiana uhamisho katika majira ya kiangazi. Meneja wa Inter
Milan, Roberto Mancini ameonyesha nia ya wazi ya kutaka kumsajili kiungo
huyo ambaye anatimiza miaka 32 Mei 13, na wakala wake Dimitri Seluk
amekiri kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka City. Seluk amesema ingawa
hakuna kilichoamuliwa mpaka sasa lakini ana uhakika wa asilimia 90 kuwa
mteja wake anaweza kuondoka katika timu hiyo majira ya kiangazi. Toure
alijiunga na City akitokea Barcelona mwaka 2010 na amefanikiwa kushinda
mataji mawili ya Ligi Kuu na moja la Kombe la FA, pia taji la Mataifa ya
Afrika akiwa na timu yake ya taifa ya Iviry Coast mapema mwaka huu.Inasemekana wenda akamfuata Robert Mancini Italia
No comments:
Post a Comment