Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lililofungwa na Awadh Juma kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu uliochezwa Uwanja wa Taifa jana |
KLABU ya Simba imehitimisha safari yake kwenye Ligi Kuu ya
Soka ya Tanzania Bara kwa ushindi baada ya kuifunga JKT Ruvu kwa mabao 2-1
kwenye mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.
Hata hivyo matokeo hayo hayana maana yoyote kwa timu hizo
kwani Simba imemaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu na hivyo kukosa nafasi ya
kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa mwakani.
Wakati JKT Ruvu yenyewe pamoja na kufungwa imefanikiwa
kubaki na pointi zake 31 na hivyo kuendelea kubaki kwenye ligi hiyo kwa msimu
ujao.
Kwenye mechi hiyo isiyoshuhudiwa na mashabiki wengi JKT Ruvu
ndio walitangulia kufunga kwa bao la Idd Mbaga aliyepokea krosi nzuri ya Ally
Bilal kwenye dakika ya 15.
Lakini bao hilo lilidumu kwa dakika nne tu kwani Simba
kupitia kwa kiungo wake Awadh Juma walifanikiwa kusawazisha bao hilo. Awadh
Juma alisawazisha bao hilo baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa JKT
Ruvu Shaabani Dihile kufuatia shuti la Emmanuel Okwi.
Dakika tatu kabla ya mapumziko Simba walifunga bao la pili
kupitia kiungo wa kimataifa wa Tanzania Said Ndemla aliyepata pasi nzuri ya
Emmanuel Okwi.
Kwenye mechi hiyo timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa kwa
Simba kumtoa Twaha Ibrahim na kumuingiza Issa Abdallah na JKT Ruvu kumtoa Idd
Mbaga na kumuingiza Cecik Ephraim.
Simba tena walimoa Wiliam Lucian na kumuingiza Mohamedi
Hussein na JKT Ruvu waliwatoa Najim Maguli na Ally Bilal na kumuingiza Abdallah
Makame lakini mabadiliko hayo hayakuweza kubadili sura ya mchezo huo.
No comments:
Post a Comment