Jumamosi zipo Mechi 7 ambazo nyingine ni muhimu kwa Timu zinazotaka kujinusuru kutoshushwa Daraja na hizo, kimahesabu, ni Timu 9 ambazo zipo kwenye hatari hiyo.
Huko juu, baada ya Chelsea kutwaa Ubingwa na kujihakikishia kuwa moja ya Timu 4 zitakazocheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao, vita imebaki kupatika 3 zipi nyingine zitaungana nao.
Ingawa Man City na Arsenal wana nafasi nzuri sana kuwemo 4 Bora, kimahesabu lolote linaweza kutokea na hivyo wanahitaji ushindi ili kujihakikishia kuwemo.
Kazi kubwa ipo kwa Man United, walio Nafasi ya 4, wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya 5 Liverpool na ambao pia, kimahesabu wanaweza kupitwa na hata Tottenham, walio Nafasi ya 6 na Southampton, walio Nafasi ya 7.
Jumamosi, Man United wako Ugenini huko Selhurts Park kuivaa Crystal Palace wakitafuta ushindi wao wa kwanza baada kudundwa Mechi 3 mfululizo.
RATIBA
Jumamosi Mei 9
14:45 Everton vs Sunderland
17:00 Aston Villa vs West Ham
17:00 Hull vs Burnley
17:00 Leicester vs Southampton
17:00 Newcastle vs West Brom
17:00 Stoke vs Tottenham
19:30 Crystal Palace vs Man United
Jumapili Mei 10
15:30 Man City vs QPR
18:00 Chelsea vs Liverpool
Jumatatu Mei 11
22:00 Arsenal vs Swansea
No comments:
Post a Comment