Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga. |
TIMU 14 ZA Ligi Kuu Tanzania Bara leo
zinashuka kwenye viwanja tofauti viwanja tofauti kumaliza mechi zao za mwisho
za kumalizia msimu wa 2014/2015.
Leo ndio itajulikana wazi timu zipi mbili
zitakazoshuka daraja baada ya bingwa na mshindi wa pili tayari kujulikana
katika kinyang’anyiro
hicho kilichoanza mwaka jana.
Yanga ndio mabingwa wapya wakati waliokuwa
mabingwa Azam FC wameshika nafasi ya pili huku Polisi Morogoro ndio iko kwenye hatari
zaidi ya kushuka daraja baada ya kushika mkia katika msimamo wa ligi hiyo yenye
timu 14.
Washindi wa Pili Tanzania Bara. |
Polisi wenye pointi 25 wanakabiliwa na
kibarua kizito dhidi ya Mbeya City, mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya.
Tayari Mbeya City yenye pointi 31 ilishajiondoa
kwenye mstari mwekundu wa kushuka, hivyo itakuwa ni kazi kwa timu hiyo ya
Morogoro. Iwapoitashinda itafikisha pointi 28, ambazo haziwezi kumvusha popote.
Lakini kama wataruhusu kufungwa pia bado ni
lazima washuke daraja. Maafande hao ambao wamekuwa wakishuka na kupanda kila
baada ya miaka kadhaa, wameshacheza michezo 25, wameshinda mitano, sare 10 na
kupoteza 10.
Timu zinazofuatana nane zikiwamo Stand
United, Mgambo Shooting, Ndanda FC na Tanzania Prisons nazo ziko hatarini kama
zitashindwa kufanya vizuri katika michezo ya leo kwa vile hufungana kwa pointi
sawa 28.
Stand United inaikaribisha Ruvu Shooting
yenye pointi 29 kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Timu hizi mbili zimetofautiana kwa pointi
moja, ambazo kama hazitashinda, moja itakuwa hatarini ikiwa nyingine
zitashinda.
Stand United wameshacheza michezo 25,
wameshinda saba, wana sare saba, wamepoteza michezo 11, hivyo wanahitaji
kushinda leo ili kuendelea kubaki kwa msimu mwingine hasa ikizingatiwa
wamepanda kwa mara ya kwanza msimu huu.
Mgambo Shooting inamaliza na Azam FC kwenye
Uwanja wa Azam Complex, Timu hii yenye maskani yake Tanga ina uwezekano wa kushuka
kama haitashinda mchezo huo mgumu kwao.
Simba mshindi wa tatu |
Tayari wameshacheza michezo 25, wameshinda nane,
sare nne na wakifanya mzaha watashuka na kuwapa nafasi African Sports iliyopanda
daraja ya kuchukua nafasi yake.
Kwa upande wa Ndanda FC inamaliza mchezo wake
na Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Timu nyingine ni Tanzania Prisons, ambayo
inacheza dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Maafande hao wanahitaji kushinda ili kuendelea kubaki na pia Kagera wanahitaji ushindi.
Michezo mingine ni kati ya Simba itakayokwaruzana
na JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, huku Coastal Union ikicheza
na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu.
Timu tano zinazofungana kwa pointi 31 ni
Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Mbeya City na Kagera Sugar.
Zote zinahitaji ushindi kujitofautisha na
zile ambazo zina pointi 28 ambazo zikishinda zinaweza kufanana na wao.
Msimamo:
Msimamo:
MP | W | D | L | GF | GA | +/- | Pts | |||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Young Africans | 25 | 17 | 4 | 4 | 52 | 17 | 35 | 55 | |||
2 | Azam | 25 | 13 | 9 | 3 | 36 | 18 | 18 | 48 | |||
3 | Simba SC | 25 | 12 | 8 | 5 | 36 | 18 | 18 | 44 | |||
4 | Mtibwa Sugar | 25 | 7 | 10 | 8 | 24 | 24 | 0 | 31 | |||
5 | Mbeya City | 25 | 7 | 10 | 8 | 21 | 22 | -1 | 31 | |||
6 | Kagera Sugar | 25 | 8 | 7 | 10 | 22 | 26 | -4 | 31 | |||
7 | JKT Ruvu | 25 | 8 | 7 | 10 | 19 | 23 | -4 | 31 | |||
8 | Coastal Union | 25 | 7 | 10 | 8 | 19 | 24 | -5 | 31 | |||
9 | Ruvu Shooting | 25 | 7 | 8 | 10 | 16 | 28 | -12 | 29 | |||
10 | Tanzania Prisons | 25 | 5 | 13 | 7 | 18 | 22 | -4 | 28 | |||
11 | Ndanda | 25 | 7 | 7 | 11 | 20 | 29 | -9 | 28 | |||
12 | Mgambo JKT | 25 | 8 | 4 | 13 | 18 | 28 | -10 | 28 | |||
13 | Stand United | 25 | 7 | 7 | 11 | 22 | 34 | -12 | 28 | |||
14 | Polisi Morogoro | 25 | 5 | 10 | 10 | 16 | 26 | -10 | 25 |
No comments:
Post a Comment