Mwesigwa
alisema kwa niaba ya TFF anaomba radhi kwa usumbufu wowote uliowapata
waandishi na wadau wote walioshindwa kushuhudia vema tukio hilo.
“TFF
na FIFA vinatambua umuhimu na nafasi ya wanahabri na vyombo vya habari
si tu katika kuutangaza mchezo, bali pia katika kutia chachu maendeleo
ya mchezo wenyewe “ alisema Mwesigwa.
Hali
mbaya ya hewa ilivuruga utaratibu uliokuwa umepangwa awali kuanzia
itifaki ya shughuli za kabla na wakati wa mchezo na zile za utoaji tuzo.
Aidha
Mwesigwa alisema TFF itaendelea kushirikiana vema na jumuiya ya
wanahabari ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wana mazingira mazuri
wanapofanya kazi kwenye matukio ya mpira wa miguu.
No comments:
Post a Comment