KIUNGO
wa Manchester City, Yaya Toure amekataa kujadili mustakabali wake
katika timu hiyo jana wakati alipoulizwa suala hilo katika uzinduzi wa
mpango mpya wa vitendo vya kibaguzi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.
Toka mwaka jana mustakabali wa Toure umekuwa katika hatihati baada ya
wakala wake Dimitri Seluk kuituhumu klabu hiyo kudharau siku yake ya
kuzaliwa huku wiki iliyopita akidai kuwa mteja wake ana uwezekano wa
kuondoka asilimia 90 katika majira ya kiangazi.Toure
ambaye ametimiza miaka 32 leo anahusishwa na tetesi za kwenda katika
klabu za Inter Milan na Paris Saint-Germain lakini mwenyewe amekanusha
taarifa hizo.Akizungumza
na wanahabari, Toure amesema alikuwa na vitu vingi vya msingi vya
kujadili na anaona in vya muhimu zaidi ya mustakabali wake katika klabu
ya City. Toure mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne,
alijiunga na City akitokea Barcelona mwaka 2010 na kuisaidia timu hiyo
kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu, moja ya Kombe la Ligi na moja la FA.
No comments:
Post a Comment