Mhariri
mkuu wa Bongo5 Bw. Fredrick Bundara (kushoto) akiwa pamoja na Mhariri
msaidizi, Sandu George wakizungumza leo na waandishi wa habari katika
uzinduzi wa Tuzo za watu 2015.
Kampuni
ya Bongo5 Media Group, imezindua msimu mpya na wa pili wa Tuzo za Watu
Tanzania zilizoanzishwa mwaka jana ili kuwatuza watu kwenye sekta ya
burudani na habari wanaofanya vizuri.
Akiongea
kwenye mkutano na waandishi wa habari leo, mhariri mkuu wa mtandao wa
Bongo5, Fredrick Bundala amesema tuzo za mwaka huu zimeboreshwa zaidi
kwa kuongeza vipengele vitatu vipya.
“Mwaka
huu tuzo zimeongezewa nguvu zaidi. Kutoka vipengele 11 tulivyokuwa
navyo mwaka jana hadi vipengele 1. Mwaka huu tumeongeza vipengele vitatu
muhimu,” amesema Bundala.
Amevitaja
vipengele vilivyoongezeka kuwa ni pamoja na muongozaji wa filamu
anayependwa, tovuti/blogu inayopendwa na mfadhili maarufu anayependwa.
“Kwenye
jamii yetu kuna watu maarufu ambao wamekuwa mstari wa mbele kusaidia
jamii hususan watu wasio na uwezo ama wanaoshi katika mazingira magumu.
Tumeona ni muhimu pia kuwatambua watu hawa ambao huamua kujinyima na
kugawana kile wanachokipata ili kuwasaidia watu wanaohitaji msaada,”
ameongeza.
Amesema
zoezi la kuanza kupendekeza majina ya washiriki limeanza rasmi Alhamis
hii ambapo wananchi wanaweza kuwapendekeza kupitia website ya www.tuzozetu.com ama kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu kwa kuandika neno TZW, code ya kila kipengele na jina la anayependekezwa kwenda 15678.
“Baada
ya wiki tatu kuanzia leo tutatangaza majina ya washiriki watano
waliochaguliwa kuingia kwenye awamu ya kwanza ya mchujo ambapo katika
kipindi cha wiki mbili itafanyika michujo mingine miwili ili kuwapata
washiriki watatu watakaoingia fainali,” amesisitiza Bundala.
“Washiriki watatu kwenye kila kipengele watahudhuria kilele cha tuzo hizo kitakachofanyika katikati ya mwezi wa tano.”
Kwa
upande wake mhariri msaidizi wa Bongo5, Sandu Mpanda, amesema kuwa
utofauti wa tuzo za watu na tuzo zingine ni kuwa wananchi wana nguvu ya
asilimia 100 kumchagua mshindi.
“Kura
za wananchi ndizo zitakazompata mshindi. Ni muhimu wananchi kuwapigia
kura watu wanaowapenda ili kuhakikisha wanashinda vipengele walivyotajwa
kuwania,” amesema Mpanda.
Mpanda
amevitaja vipengele vinavyowaniwa kwenye tuzo za mwaka huu kuwa ni
pamoja na Mtangazaji wa redio anayependwa (TZW1), Kipindi cha redio
kinachopendwa (TZW2), Mtangazaji wa kipindi cha runinga anayependwa
(TZW3), Kipindi cha runinga kinachopendwa (TZW4), Tovuti/Blogu
inayopendwa (TZW5) na Muongozaji wa video za Muziki anayependwa (TZW6).
Vingine
ni Muongozaji filamu anayependwa (TZW7), Mwigizaji wa kike anayependwa
(TZW8), Mwigizaji wa kiume anayependwa (TZW9), Mwanamuziki wa kike
anayependwa (TZW10), Mwanamuziki wa kiume anayependwa (TZW11), Filamu
inayopendwa (TZW12), Video ya Muziki inayopendwa (TZW13) na Mfadhili
maarufu (TZW14).
Hashtag za kwenye mitandao ya kijamii mwaka huu ni #TZW2015 na #TuzozaWatu.
Kwa hisani ya Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment