SENEGAL
itakutana na Nigeria katika fainali ya Vijana 2015 baada ya kuifunga Mali 2-1
na kushinda katika mchezo wa nusu fainali ya pili Alhamisi.
Wenyeji
walitinga nusu fainali kama washindi wa pili katika Kundi A lakini hiyo
haikujalisha baada ya kukutana na Mali ambao ni washindi wa kwanza wa Kundi B.
Ulikuwa
mchezo wa kuvutia sana wakati timu hizo mbili zilipochuana vikali huku Moussa
Kone akifunga bao la kuongoza mwanzoni kabisa mwa mchezo. Bao hilo liliwapa
nguvu wenyeji Senegal ikiwa ni kama sekunde 57 tu tangu kuanza kwa mchezo huo.
Kipa wa Mali
Sory Ibrahim Traore hakuweza kulizuia shuti hilo na mpira kumkuta Kone na
kufunga bao la kwanza kati ya mawili.
Hata hivyo,
Mali walijibu mapigo haraka na dakika moja baadae walifanikiwa kusawazisha na
kufanya timu hizo kuwa sare kwa bao la mpira wa mbali lililofungwa na Alhassane
Diallo huko Ibrahima Sy, akiwa katika goli la Senegal asijue la kufanya.
Senegal,
ambayo haijawahi kufuzu kwa mashindano ya Fifa ya wachezaji wenye umri chini ya
miama 20, iliendelea kuweka shinikizo, lakini Mali ndio nusura wapate bao
katika dakika ya 36 kupitia kwa Saliou Guindo.
Kipindi cha
pili kilishuhudia timu zote zikifanya mashambulizi kwa zamu wakati shuti la
Mohamed Guilavogui lilipookolewa na Sy, baada ya kufanya kazi nzuri.
Senegal
ilipata bao la ushindi katika dakika 80 lililofungwa tena na Kone na kuiwezesha
timu hiyo kutinga fainali hiyo ya Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri
chiniya miaka 20.
No comments:
Post a Comment