KOCHA Arsene
Wenger amesisitiza kuwa hakuna mgogoro wa soka la England Ulaya licha ya mwaka
wa pili mfululizo kwa timu za nchi hiyo kutolewa katika hatua ya 16 bora katika
mashindano ya Ligi ya Mabingwa, lakini anaamini kua wakati umefika wa kubadili
mfumo wa sheria ya bao la ugenini.
Arsenal na
Chelsea zote zilitolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa
faida ya bao la ugenini katika hatua ya kwanza ya mtoano, zikifungwa na Monaco
na Paris Saint-Germain.
Hata hivyo,
Wenger, amekuwa kwa muda mrefu akipigania kubadilishwa kwa sheria hiyo.
'Hiyo ni
sheria iliyopitwa na wakati na sasa wakati umefika wa kuibadilisha, ' alisema
kocha huyo wa Arsenal. 'Labda sheria hiyo ituike baada ya kuchezwa muda wa
nyongeza. Ilianzishwa miaka 1960 ili kuziwezesha timu kushambulia zikicheza
ugenini.
'Tangu
wakati huo ilipoanzishwa sheria hiyo soka limebadilika sana na uzito wa bao la
ugenini kwa sasa ni mkubwa sana. Labda bao hilo lihesabike baada ya muda wa
nyongeza kama vile katika Kombe la Ligi England.
'Nafikiri
kiwango cha Ligi Kuu ya England ni kikubwa na siko katika hali ya kuelezea sana
nini tatizo la soka la Uingereza. Sifiiri kama kuna tatizo kubwa'
Wenger sasa
anatakiwa kuwaweka tayari wachezaji wake kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi wa
Ligi Kuu ya England dhidi ya Newcastle United wakati mpambano wa kusaka nafasi
nne za kwanza ukiendelea katika ligi hiyo.
Aliongeza:
'hali iko chini ya tumekatishwa tamaa. Mpambano ulidumu kwa takribani dakika
180 na hatukuwa na tahadhari ya kutosha katika dakika 90 za kwanza. Tunajua
kwanini tumetolewa, ni tatizo ka kuzuia katika mchezo wa kwanza.
SHERIA YA
GOLI LA UGENINI:
Endapo mpira
utamalizika watimu hizo zikilingana magoli, timu iliyofunga mabao mengi ugenini
itatangazwa kuwa mshindi wa mchezo huo.
Mfano,
Monaco iliifunga Arsenal 3-1 ugenini kabla ya kufungwa 2-0 huko Monte Carlo.
Huku matokeo
yakiwa bao 3-3, Monaco imesonga mbele baada ya kufunga goli nyingi zaidi
ugenini ukilinganisha na bao mbili za Arsenal ugenini.
No comments:
Post a Comment