Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, March 24, 2015

MARTIN SKRTEL KUADHIBIWA NA FA, KISA KIPA DAVID DE GEA WA MAN UNITED


BAADA ya machungu ya kutandikwa 2-1 kwao Anfield na Mahasimu wao Man United Jumapili na pia Kepteni wao Steven Gerrard kupewa Kadi Nyekundu katika Mechi hiyo hiyo na sasa kufungiwa Mechi 3, balaa kwa Liverpool bado halijaisha kwani sasa FA imemfungulia Mashitaka Sentahafu wao Martin Skrtel kwa kumkanyaga Kipa wa Man United David De Gea katika Mechi hiyo hiyo.Kwa vile tukio hilo la Skrtel, ambalo lilitokea Dakika za Maheruhi halikuonwa na Refa Martin Atkinson, Kanuni za FA, Chama cha Soka England, zinataka Jopo Huru la Marefa Watatu wa zamani walipitie na ikiwa wote Watatu wataafiki linastahili Kadi Nyekundu basi Mchezaji husika hufunguliwa Mashitaka.Steven Gerrard akioneshwa kadi nyekundu na Mwamuzi.
Hayo ndio yaliyomkuta Skrtel, Mchezaji wa Kimataifa wa Slovakia mwenye Miaka 30, ambae amepewa hadi Leo Saa 3 Usiku kujibu Shitaka lake.
Ikiwa atapatikana na hatia, Sentahafu huyo atafungiwa Mechi 3 na atazikosa Mechi 2 za Ligi Kuu England za Aprili 4 huko Emirates na Arsenal na ile ya Anfield na Newcastle hapo Aprili 14 na Marudiano ya FA CUP ya Robo Fainali huko Ewood Park na Blackburn Rovers hapo Aprili 8. Hizo pia ndizo Mechi ambazo Kepteni Steven Gerrard atazikosa baada ya Kadi Nyekundu kwenye Mechi hiyo hiyo aliyolambwa Sekunde 38 tu tangu aingie Uwanjani kutoka Benchi kwa kumkanyaga kwa kusudi Ander Herrera wa Man United.

No comments:

Post a Comment