Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangza
viingilio vya mchezo wa siku ya jumapili kati ya Taifa Stars (Tanzania) dhidi
ya The Flames (Malawi) utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
kuwa ni tsh. 5,000 mzunguko na tsh. 12,000 kwa jukwa kuu.
Kuelekea mchezo huo wa jumapili kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, kimeendelea na mazoezi
katika Uwanja wa CCM Kirumba huku wachezaji wake wote wakiwa na ari na morali
ya juu tayari kwa kuwakabili the Flames.
Taifa Stars iliyo chini ya kocha mkuu Mart Nooij iliwasili
jijini Mwanza siku ya jumanne na kufikia katika hoteli ya La Kairo iliyopo eneo
la Kirumba,
ikiwa na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa
Kimataifa uliopo kwenye kalenda ya FIFA.
Maandalizi ya mchezo kwa upande wa Taifa Stars yamekamilika,
timu imekua ikifanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba ambao ndio uwanja
utakaotumika kwa mchezo.
Wachezaji waliopo jijini Mwanza ni , Aishi Manula, Mwadini
Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Nadir Haroub,
Salim Mbonde, Haji Makame, Hassan Isihaka na Abdi Banda.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Haroun Chanongo, Mrisho Ngasa,
Salum Abubakar, Amri Kiemba, Frank Domayo, Said Ndemla, John Bocco, Juma
Luizio, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
No comments:
Post a Comment