Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O Afrika uliofanyika jumamosi uwanja wa ndani wa Taifa. Class alinyakuwa ubingwa huo kwa kushinda kwa Pointi na sasa Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Afrika wa W.P.B.F na U.B.O Africa |
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwa na mikanda yake ya ubingwa wa Africa wa U.B.O na WPBF |
Bondia Cosmas Cheka akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Afrika |
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akishangilia ushindi na mashabiki wake baada ya mpambano wake na Cosmas Cheka |
BONDIA
Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ametwaa ubingwa wa U.B.O Afrika kwa kumpinga
bondia Cosmas Cheka wa Morogoro kwa pointi katika pambano la raundi kumi
lililofanyika katika Uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Pambano lilianza kwa mashambilizi ya kushtukiza huku kila bondia akimtupia makonde mwenzie jambo lililofanya kuwa wa vuta nikuvute kwa kila mmoja kwani walijiandaa kwa muda mrefu lakini mwishowe Class akaibuka kidedea baada ya raundi kumi kumalizika
Akizungumza
baada ya pambano hilo bondia, Ibrahim Class alisema anamshukuru Mungu kwa
kumwezesha kushinda pambano hilo kwani mpinzani wake naye alikuwa mzuri.
“Cheka siyo
bondia wa kumfanyia masihara kama sikujiandaa vizuri angeweza kunipiga kwani
ngumi zake nzito lakini namshukuru Mungu nimeshinda”, alisema Class.
Katika mapambano mingine iliyopigwa bondia Fadhili Majiha alimpiga Francis Miyeyusho kwa pointi huku Vicent Mbilinyi na Epson John wa Morogoro kumaliza kwa sare.
Bondia
Shedrack Ignas alimpiga bondia Husein Mbonde kwa KO ya raundi ya nne ya pambano
naye Saidi Mundi akimpiga kwa pointi bondia Ramadhani Shauri
Mashabiki waliofika kuona pambano huo wameomba mapambano yawe yanaanza mapema kuondoa hadha ya usumbufu wa usafiri wakati wa kurudi kwenda majumbani kwani wengi wanategemea usafiri wa daladala
Mashabiki waliofika kuona pambano huo wameomba mapambano yawe yanaanza mapema kuondoa hadha ya usumbufu wa usafiri wakati wa kurudi kwenda majumbani kwani wengi wanategemea usafiri wa daladala
No comments:
Post a Comment