Mlango umefunguliwa kwa Vermaelen wakati huu Manchester United na Barcelona wakihusishwa. |
Arsene
Wenger amesema kuwa mlinzi wa kati na nahodha wake Thomas Vermaelen
anaweza akaondoka Arsenal, wakati huu ambapo Manchester United
wakiendelea kuonyesha nia ya kumsajili.
Wenger,
akiongea
kuelekea katika ushiriki wao wa Emirates Cup mwishoni mwa wiki hii
amesema anategemea mlinzi huyo wa kati wa Belgium atasalia klabuni
lakini pia anayo nafasi ya kuondoka.
Menejea huyo wa washika mitutu amesema
'Ni majeruhi kwasasa, lakini kuna uwezekano pia akaondoka lakini nategemea atabaki ni mchezaji mzuri.'
Vermaelen anawindwa na meneja Manchester United Louis van Gaal lakini pia amekuwa akihusishwa na kuelekea Barcelona.
Wenger
pia ametupilia mbali juu ya tetezi za kutaka kuwasajili Mcolombia Juan Quintero na Mario Balotelli.
Wenger alikuwa akiongea kuelekea Emirates Cup, Arsenal michuano ya mwishoni katika maandalizi ya msimu
Wenger anajipanga kumbadilisha Calum Chambers kucheza ulinzi wa kati
Jack Wilshere amekuwa katika hali nzuri kimchezo katika kipindi cha miaka mitatu anasema Wenger
No comments:
Post a Comment