Lionel Messi hakuwa na tabasamu baada ya mchezo wa fainali ya kombe la dunia lakini kwasasa anafanya hivyo.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Argentina ametupia picha mtandaoni akiwa na mpenzi
wake Antonella Roccuzzo, ambapo wapenzi hao walivinjari katika kisiwa
cha maraha cha Capri kilichoko nchini Italia.
Roccuzzo
alikuwepo nchini Brazil akifurahia kwa pamoja tuzo ya mchezaji bora wa fainali za kombe la dunia 'Golden
Ball' pamoja na kwamba kikosi cha Argentina kilipoteza katika fainali dhidi ya Ujerumani.
Lionel Messi (kushoto) na mpenzi wake Antonella Roccuzzo (kulia) wakati wa mapumziko yao kisiwania Capri nchini Italia.
Picha ya selfie: Messi (kushoto) akiwa na Roccuzzo (kulia) na mtoto wao wa kiume Thiago (katikati)
Pozi safi: Messi akiwa katika shopping duka la Dolce & Gabbana pamoja na Antonella Roccuzzo
Messi
bado hajaungana na kikosi cha Barcelona kilichoko katika maandalizi ya
msimu mpya ambapo watacheza mchezo dhidi ya Nice ya Ufaransa Agosti 8.
No comments:
Post a Comment