Mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu baina ya vilabu vya Simba na
Mbeya City uliokuwa unachezwa hivi punde huko jijini Mbeya katika dimba
la Sokoine umemalizika.
Matokeo ya mchezo huo ni sare ya bao moja kwa moja, Mbeya City ndio
walioanza kuliona lango la Simba katika dakika ya 13 kwa mkwaju wa
penati likifungwa na Deogratius Julias , bao hilo lilidumu mpaka mapumziko wenyeji wakitoka kifua mbele.
Kipindi
cha pili Simba walianza kwa kasi na hatimaye katika dakika ya 50,
mshambuliaji hatari wa Simba Mrundi Amiss Tambwe akaifungia timu yake
bao la kusawazisha.
Timu hizo ziliendelea kushambuliana lakini mpaka refa anapuliza
kipenga cha mwisho matokeo yalibaki moja kwa Mbeya City na moja kwa
Simba.
KUTOKA COMORO
Mabingwa
wa Tanzania bara na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kombe la
mabingwa wa Afrika Dar Young African imefanikiwa kuvuka kwenda raundi ya
pili ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Komorozine De Domoni
mabao 5-2.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Mrisho Ngassa aliyefunga hat trick, huku Hamis Kiiza na Msuva wakifunga bao moja moja.
Yanga sasa watakutana na timu kubwa ya Misri Naciona Al Ahly.
No comments:
Post a Comment