Mario Balotelli jana
ameipa ushindi AC Milan baada ya kufunga bao la dakika za lala salama dhidi ya Bologna
katika mchezo wa Serie A.
Balotelli alifunga bao lake hilo la 10 msimu huu kwa shuti
la umbali wa mita 30 dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho na kuipandisha Milan
hadi nafasi ya 10 kwa kufikisha pointi 32 sawa na Lazio iliyo nafasi ya tisa.
Lakini Balotelli hakulishangilia bao hilo zaidi ya
kukumbatiwa na wachezaji wenzake.
No comments:
Post a Comment