MABONDIA 21
wakiwemo wanawake wanne wameteuliwa kuunda timu ya ngumi za ridhaa ya mkoa wa
Dar es Salaam itakayoshiriki mashindano ya majiji yatakayofanyika Kampala,
Uganda kuanzia Aprili 2 hadi 9 mwaka huu.
Mwenyekiti
wa Chama cha ngumi Mkoa wa Dar es Salaam, Akaroly Godfrey alisema kuwa mabondia
hao watafundishwa na makocha wanne watakaoongozwa na Frednand Nyagawa
atakayesaidiwa na Anthony Kameda, David Yomba Yomba na Mazimbu Ally.
Mabondia hao
ni Mussa Mchomanga (JKT), Omary Said (Green House) na Anthony Idoa (Magereza)
watakaocheza uzito wa lightfly.
Katika uzito
wa fly waliochaguliwa ni Hafidh Bamtula (Azimio), George Costantine (MMJKT)
wakati katika uzito wa bantam waliochaguliwa ni Emilian Patrick (Mgulani JKT),
Hamad Furahisha (Magereza) na Undule Lagson.
Uzito wa
light waliochaguliwa ni Alex Michael (MMJKT) na Kassim Mbutike (MMJKT), katika
uzito wa lightwelter ni Victor Njaidi , Haruna Hussein (Mgulani JKT) na Seleman
Bamtula (Azimio). Katika uzito wa welter ni Mohamed Kibumbuli (Magereza) na
Mussa Seif (Mavituuz).
Kwa upande
wa uzito wa middle ni Hamidu Klahlfan (MMJKT) wakati uzito wa heavy ni Joseph
Martin.
Kwa upande
wa wanawake ni Grace Mwakamela, Sarah Andrew, Irine Mushin a Siwatu Kinde wote
wa Makamo Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (MMJKT)huku daktari wa timu hiyo ni
Mussa Maila.
No comments:
Post a Comment