Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 17, 2014

SEMSEKWA NA SHARAPOVA WAPAGAWISHA MEEDA



 
RAPA mpya wa Extra Bongo Grayson Semsekwa na mnenguaji Asha Sharapova  walikonga nyoyo za mamia ya mashabiki wa muziki wa dansi waliojitokeza katika onyesho maalum la utambulisho wa wanamuziki hao lililofanyika katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam. 

Semsekwa na Sharapova walitangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita kujiunga na Extra Bongo wakitokea bendi hasimu ya African Stars Twanga Pepeta tayari kujiandaa na uzinduzi wa albamu mpya ya bendi hiyo inaoitwa Mjini Mipango itakayozinduliwa Februari 22 mwaka huu katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala. 

Mara baada ya Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki kumpandisha jukwaani rapa huyo na kuanza kuimba vipande vya rapu zake za kwenye nyimbo za zamani kama Regina Zanzibar, Double Double, 3x3 mashabiki walijikuta wakishindwa kutulia kwenye viti na kwenda kumtunza hali iliyofanya ukumbi kuchangamka kwa mayowe ya furaha. 

Kwa upande wake Sharapova alionyesha umahiri wa kunengua sambamba na wenzake katika shoo maalumu ya kinadada ambapo licha kutofanya nao mazoezi aliweza kuendana na staili za mtindo mpya wa bendi hiyo 'Kimbembe'. 

Wanamuziki hao wanaonguna na wenzao tayari kuingia kambini wiki hii kujiwinda na uzinduzi wa albamu ya 'Mtenda Akitendewa' unaosuburiwa kwa hamu na mashabiki wa muziki wa dansi. 

Mtenda Akitendewa ni albamu ya nne kwa bendi hiyo iliyoasisiwa kwa mara kwanza mwaka 2003 ikiwa na waimbaji Ally Choki, Bashiri Uhadi, Bob Kissa, Richard Maarifa, Khalidi Chokoraa, Flora Moses, rapa Greyson Semsekwa.

Wengine ni Bonzo Kwembe anapiga Solo, Efraim Joshua,George Gama wanapiga besi, Rythm na Thabit Abdul anayepiga kinanda na Imma Chokolate anayepiga ngoma. 

Albamu ya kwanza iliitwa '3x3' ambao ni wimbo uliokuwa kwenye albamu nyimbo nyingine ni 'Regina Zanzibar', 'Tuchunge Wazazi au Fikiri Madinda', 'Nunu Milenium' 'Walimwengu Remix' na 'Odise'. 

Albamu ya pili ilitwa 'Bullet Proof' ikiwa na nyimbo kama 'Double Double' na 'Regina Zanzibar' kabla ya kusambaratika mwaka 2004 na bendi hiyo kuanzishwa tena mwaka 2009 na kuibuka na 'Mjini Mipango

No comments:

Post a Comment