Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, February 17, 2014

KOCHA WA NGUMI REMMY NGABO AULA DABA


 


CHAMA cha Ngumi za Ridhaa mkoa wa Dar es Salaam kimemteua aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya ndondi ya taifa Remmy Ngabo kuwa, Mkurugenzi wa Ufundi na Maendeleo ya Wachezaji.

Shirikisho la Ndondi Tanzania BFT hivi karibuni lilimtema Ngabo mwenye cheti cha daraja la kwanza cha ufundishaji ndondi pamoja na makocha wengine kuifundisha timu hiyo na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Selemani.

Akizungumza jijini Mwenyekiti wa DABA Akaroly Godfrey alisema kuwa wamemteua Ngabo kuwa mkurugenzi wa ufundi ili awasaidie katika kuuendeleza mchezo huo hapa Dar es Salaam.

Awali, ilidaiwa kuwa, Ngabo aliingia matatani na uongozi wa BFT baada kocha huyo kuudhuria Uchaguzi Mkuu wa chama cha mkoa wa Dar es Salaam, ambao BFT walidai kutoutambua na baadae kushiriki katika mashindano yaliyoandaliwa na mkoa huo.

Mashindano hayo ya wazi ya mkoa wa Dar es Salaam yalifana huku yake ya taifa ya wazi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers kutokuwa na msisimko baada ya baadhi ya mabondia nyota kutoshiriki mashindano hayo.




No comments:

Post a Comment