MABONDIA
Japhet Kaseba na Thomas Mashali wametambiana kila mmoja kumpiga mwenzake mbele
ya mashabiki waliofika kushuhudia pambano la kusheherekea siku nya wapendanao
lililofanyika katika Ukumbi wa Mpo Afrika Temeke Dar es Salaam.
Mabondia hao
walionesha dhahiri kutamani kupigana kwani walifika mahali kusema kama kuna
promota anayetaka kuandaa pambano kati yao awaone ili wakubaliane.
“Mimi
nakutamani kupigana na wewe hata sasa hivi kwani ulingo upo hapa ili
nikufundishe ngumi zinavyopiganwa maana unatamba sana kwa vile unakutana na
mabondia nyanya”, alisema Kaseba.
Kwa upande
wa Mashali yeye alisema yupo tayari kupigana na Kaseba mahali popote kwani
anajiamini atampiga kwa KO katika raundi za mwanzo tu.
Maneno ya
mabondia hao yaliwavuta mashabiki waliofika ukumbini hapo kujionea mapambano
yasiyokuwa na ubingwa ambayo yalikuwa maalum kusheherekea siku ya wapendanao na
kutamani wangepanda ulingoni muda huo.
Japhet
Kaseba ambaye aliwahi kuwa bingwa ngumi za mateke na baadae kuhamia kwenye
ngumi za kulipwa ameshacheza mapambano
nane na kushinda matano huku matatu akishinda kwa KO na kupigwa kwa KO
mapambano matatu.
Kwa upande
wa Mashali ameshacheza mapambano 12 na kushinda mapambano tisa huku matano
akishinda kwa KO, moja akatoka sare na kupigwa kwa KO mapambano mawili.
No comments:
Post a Comment