LIGI daraja
la tatu mkoa wa Tabora hatua ya nane bora inatarajiwa kuanza kutimua vumbi
Februari 23, mwaka huu katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Vita, Tabora.
Akizungumza
kwa njia ya simu toka Tabora, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
(TAREFA) Fate Remtullah alisema kuwa ligi hiyo itahusisha timu nane kutoka
katika vituo vitatu.
“Ligi ya
daraja la tatu hatua ya nane bora itaanza kuchezwa Februari 23, mwaka huu
katika Uwanja wa Vita na hatutasikiliza sababu ya timu kushindwa kufika kwenye
mchezo wake kwani tunataka tuwahi tarehe ya mwisho ya majina ya mabingwa TFF”,
alisema Remtullah.
Msimu
uliopita Tabora pamoja na baadhi ya mikoa iliathiriwa na mabadiliko ya mfumo wa
uendeshaji wa ligi ikasababisha ligi kuchezwa kama bonanza ili kupata
mwakilishi wa mkoa.
Timu
zilizoingia kwenye hatua ya nane bora ni Reli Goweko FC, Mirambo FC, Magereza
FC, Nzega FC, Abajalo FC, Manchester FC, Warumba FC na Chipukizi FC.
Pia
alizishukuru timu zote zilizoshiriki ligi katika hatua ya makundi katika vituo
vya Manispaa, Igunga na Sikonge pamoja na waamuzi kwa kufanikisha makundi
kumalizika salama bila malalamiko.
No comments:
Post a Comment