TIMU ya
Black Eagle imeifunga Ilala FC bao 1-0 katika mchezo wa ligi daraja la nne
Manispaa ya Iringa, mchezo uliochezwa Uwanja wa Samora.
Bao la Black
Eagle katika mchezo huo lilifungwa na Hashim Chang’a katika dakika ya 10, bao
ambalo lilidumu hadi dakika 90 ya mchezo.
Katika
mchezo mwingine Isakalilo FC ilitoka sare ya kutofunga na Real FC katika mchezo
uliochezwa uwanja wa Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa.
Akizungumza
kwa simu toka Iringa, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Manispaa ya Iringa, (IMFA)
Rashid Shungu alisema kuwa ligi inaendelea vizuri kwani hawajapata malalamiko
kuanzia ianze kuchezwa.
“Ligi yetu
inaendelea vizuri na nashukuru hakuna malalamiko ambayo yamewasilishwa katika
ofisi yangu hivyo naamini ligi itamalizika kama ratiba ilivyopangwa”, alisema
Shungu.
Ligi hiyo
inayofadhiliwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) Fredrick Mwakalebela inatajiwa kuendelea kesho kwa kuzikutanisha timu za Mtwa
FC na Mtwivila City.
No comments:
Post a Comment