
Msanii
wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange mwenye maskani yake mjini
Morogoro,ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka
Morogoro leo usiku atakuwa kwenye jukwaa moja na msanii wa muziki Cindy
Sanyu kutoka Nchini Uganda katika usiku wa wapendanao (Valentine Day)
leo Ijumaa katika Ukumbi wa JB Belmonte Hotel (Serengeti Hall). Wasanii
hawa wawili hawatakuwa wao peke yao pia kutakuwepo na wasanii wengine
kama Zedy Y, K Fan, Dogo D, na Mwanza Rainbow Dancers.

Msanii
wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange (kulia) akiwa na Msanii mwenzake
kutoka Nchini Uganda Cindy Sanyu leo katika ukumbi wa JB Belmonte Hotel
wa jijini Mwanza. Tayari kwa kutoa Burudani kali leo siku ya wapendanao
(Valentine Day 2014).

Msanii
Cindy Sanyu kutoka Uganda (kushoto) katikati ni Promota wao Bw. Baraka
Nyororo na kulia ni msanii wa Bongo Flava wa hapa Nchini Tz Dayna
Nyange.

Cindy Sanyu na Dayna Katika picha ya Pamoja.

Picha ya wasanii na Promota wao.
Post a Comment