KOCHA WA MAN UNITED AANZA VISINGIZIO, ALIA NA WAAMUZI
MENEJA
wa klabu ya Manchester United, David Moyes amelalamika kuwa kikosi
chake mbali na kucheza na timu pinzani lakini pia kinacheza dhidi ya
waamuzi baada ya kufungwa mabao 2-1 na Sunderland katika mchezo wa
mkondo wa Kombe la Ligi uliochezwa jana. Moyes ambaye yupo katika
shinikizo baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo katika mashindano yote
alimnyooshea kidole mwamuzi Andre Marriner ambaye alitoa adhabu ndogo
iliyowapa Sunderland bao la kwanza.
Moyes akiwa mazoezini na Vijana kazi wake!
Kipa David de Gea akiwa kwenye mawazo mengi hapa!
Captain Nemanja Vidic jana baada ya kufungwa na Sunderland
Fabio alitupwa nje kwa kadi nyekundu wakati United wanacheza na Swansea hivi karibuni.
Post a Comment