Uganda
Cranes itawakosa mlinzi Godfrey Walusimbi na mshambuliaji nyota
Emmanuel Okwi kwenye fainali zijazo za mataifa ya Afrika kwa wachezaji
wa ndani CHAN nchini Afrika kusini kufuatia taarifa ya shirikisho la
soka Afrika (CAF) kusema wachezaji hao wamekosa uhalali kwani bado wana
mikataba na vilabu vyaoa vya nje ya nchi yao.
Bodi
ya mashindano ya CAF ilikuwa ikijibu maombi ya mapema ya shirikisho la
soka nchini Uganda FUFA yaliyo kuwa yakitaka ufafanuzi juu ya uwezekano
wa kupatikana kwao kwenye fainali hizo.
Okwi
na Walusimbi ambao kwasasa wanaichezea Sports Club Villa ya Uganda
waliviacha vilabu vya katika mazingira ya sintofahamu huku madai yao
makubwa yakiguzia kuvunjwa kwa masharti ya mikataba yao na vilabu vyao
lakini baadaye CAF na FIFA wakawapa idhini ya kuchezea vilabu vya
nyumbani kwao.
Okwi
aliiacha klabu yake ya Etoile Du Sahel ya Tunisia kwa madai ya
kutokulipwa pesa yake yote ya usajili huku Walusimbi akishindwa kurejea
tena DR Congo katika klabu yake ya CS Don Bosco baada ya kuitumikia timu
ya taifa ya Uganda Cranes dhidi ya Liberia kwenye mchezo wa kuwani
kufuzu kombe la dunia 2014 akieleza kuwa hakukuwa na malezi mazuri ndani
ya klabu hiyo.
Ingawa
CAF iliwaruhusu kuchezea SC Villa, taarifa zinadai kuwa wawili hao bado
wana mikataba na vilabu vyao hivyo na kwamba wanachezea SC Villa kwa
mkopo.
Kwa mujibu wa taarifa kupitia mtandao wa habari za michezo wa Kawowo Sports
nchini Uganda juhudi za kumpata mtendaji mkuu wa FUFA Edgar Watson zinaendelea kutoa muendelezo wa taarifa hii.
Uganda iko katika kundi B pamoja na Morocco, Burkina Faso na Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment