Wachezaji hao walitwaa Ubingwa wa Dunia kwa kuilaza Mexico bao 3-0 Ijumaa iliyopita mjini Abudhabi.
Rais Goodluck Jonathan pia aliahidi kutoa nishani za kitaifa kwa viongozi wa timu timu hiyo huku akiagiza wadau mbali mbali kutoka sekta binafsi kumuunga mkono katika kuizawadia Timu hiyo.
Katika Mapokezi ya Timu hiyo Mjini Abuja,Rais Jonathan alisema Huu ni ushindi wenu halali na wa kujivunia.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa Ushindi huo wa Vijana ni mwanzo mpya wa kufufua moyo wa ushindani nchini Nigeria.
Katika Kipindi cha Miezi saba Timu hii imetoka nafasi ya pili kwa ubora barani Afrika hadi kuwa nafasi ya kwanza kwa ubora duniani.
Mwaka 2007,aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Umaru Yar’adua aliwazawadia kila mchezaji nyuma ya vyumba vitatu baada ya kutwaa Ubingwa wa Dunia kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 17 nchini Korea Kusini.
Wachezaji hao pia walizawadiwa nishani ya juu ya heshima nchini Nigeria kutokana na ushindi huo.
Rais Jonathan ametoa wito kwa shirikisho la soka la Nigeria NFA kuwaendeleza vema wachezaji hao ili hatimaye waweze kuichezea Timu ya taifa ya wakubwa ya Nigeria Super Eagles.
Hata Hivyo Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Nigeria Steven Keshi amesema si vema kuwalazimisha wachezaji hao kuichezea Timu ya taifa ya wakubwa.
Kocha huyo ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa Timu ya taifa ya soka ya Nigeria alisema kuwa binafsi angependelea wachezaji kufuata njia ya kawaida na kukua kiuchezaji ili wachezee timu ya umri chini ya miaka 20 na 23 na hatimaye ndipo waweze kupandishwa kuchezea kikosi cha Super Eagles hususan kwa wale watakaokuwa wameonyesha uwezo mkubwa.
Hii ni mara ya nne kwa Timu ya taifa ya Nigeria chini ya umri wa miaka 17 kutwa Ubingwa wa Dunia baada ya kufanya hivyo mwaka 1985 nchini China,Mwaka 1993 nchini Japan,2007 korea kusini na mwaka huu 2013 Falme za Kiarabu.
No comments:
Post a Comment