Mji wa Munich hautawania kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya majira
ya baridi baada ya kushindwa kuungwa mkono na wakaazi wa mji huo katika
kura ya maoni kuhusiana na iwapo mji huo uliingie katika kinyang'anyiro
cha kuwania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Meya wa jiji la Munich
Christian Ude amesema kuwa juhudi za kuwa wenyeji wa michezo hiyo ya
mwaka 2022, zimeshindwa baada ya wilaya zote pamoja na eneo la milima ya
Alpine la Garmisch-Partenkirchen na Munich kupiga kura dhidi ya juhudi
hizo baada ya mji wa Munich kuomba bila mafanikio kuwa mwenyeji wa
mashindano ya mwaka 2018.
Ludwig Hartmann ni mwenyekiti wa wabunge wa chama cha kijani cha walinzi
wa mazingira katika bunge la jimbo la Bayern na ambaye alikuwa akifanya
kampeni dhidi ya uenyeji wa jiji la Munich katika michezo hiyo ya
Olimpiki ya majira ya baridi. Hartmann amesema huu ni ushindi dhidi ya
wanaotaka kufaidika na michezo hii.
"Kwa kweli hii si ishara dhidi ya michezo, ni ishara ya wazi kabisa
dhidi ya hali ya kutokuwa na uwazi, dhidi ya watu wa kamati ya kimataifa
ya Olimpiki IOC wanaotaka kufaidika na michezo hii, na leo ni siku
ambayo viongozi wa kamati ya kimataifa ya Olipmiki wamepata pigo na sio
pigo kwa michezo."
Munich ilijaribu kuwa mji wa kwanza kuwa mwenyeji wa mashindano ya
majira ya joto na majira ya baridi ya Olimpiki, baada ya kuwa mwenyeji
wa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka 1972.
Wakati huo huo mwenge wa olimpiki kwa michezo ya mwaka 2014 ya majira ya
baridi mjini Sochi umerejea duniani mapema leo.
Chombo cha anga
kilichowachukua wanaanga wa Urusi Fyodor Yurchikhin , mwanaanga wa
Marekani Karen Nyberg na Mtaliani Luca Parmitano kilitua salama leo
nchini Khazakhistan, hizi zikiwa ni taarifa kupitia shirika la mambo ya anga la Marekani NASA.
Mwenge huo ulichukuliwa na wanaanga wawili katika mbio za kwanza za
mwenge huo angani siku ya Jumamosi.
Na kwa taarifa hiyo ndio sina budi kusema tumefikia mwisho wa kuwaletea
habari hizi za michezo jioni ya leo. Jina langu ni Sekione Kitojo , hadi
mara nyingine kwaherini.
No comments:
Post a Comment