Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 8, 2013

WENGER NA RAMSEY WASHINDA TUZO YA MWEZI UINGEREZA



 

KIUNGO MAHIRI WA KLABU YA ARSENAL, AARON RAMSEY AMESHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI SEPTEMBA WA LIGI KUU NCHINI UINGEREZA HUKU MENEJA WA KLABU HIYO ARSENE WENGER AKICHUKUA TUZO YA KOCHA BORA WA MWEZI. 

RAMSEY AMEFUNGA MABAO MANNE KATIKA BAADHI YA MECHI ZA ARSENAL MWEZI ULIOPITA YAKIWEMO MABAO MAWILI ALIYOFUNGA KATIKA MECHI YA UGENINI DHIDI YA SUNDERLAND NA MENGINE DHIDI YA STOKE CITY NA SWANSEA CITY.  

KWA UPANDE WA WENGER YEYE AMEKIWEZESHA KIKOSI HICHO KUONGOZA LIGI HIYO KWA KUSHINDA MECHI NNE MFULULIZO IKIWEMO USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA MAHASIMU WAO KUTOKA KASKAZINI MWA JIJI LA LONDON TOTENHAM HOTSPURS. 

\MECHI YA LIGI INAYOFUATA KWA ARSENAL NI DHIDI YA NORWICH OCTOBA 19 BAADA YA KUMALIZIKA KWA MECHI ZA TIMU ZA TAIFA


No comments:

Post a Comment