YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi
karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi
yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa
kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3
(mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football
Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati
ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:
1. bodi ya TPL
1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa
kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika
mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa
kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja
aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2.
utaratibu wa dunia nzima
2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya
kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji
wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani.
2.2 Mfumo (undertaking) ambao TPL
inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na
Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.
2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam
Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu
zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa
michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote
kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya
timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.
2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA
siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao
hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi,
lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1
Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa
washabiki wengi;
2.4.2
Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na
Wanachama;
2.4.3
Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku
kutoka Serikalini n.k.
3.
MIGOGORO YA
MASLAHI
3.1
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL
ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya
TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2 Makampuni
ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji
wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu
zaidi kuliko mprira wa miguu, kama vile
Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na
msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira
wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.
3.3 Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati
MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa
Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama
Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.
4. KUTOKUWA NA UWAZI
4.1 Mkataba wa
utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa
na vyombo vingi vya habari, na vyombo
ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa
kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi
Kuu (Tanzania Premier League).
4.2 Ukosefu wa
uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL
haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya
ombi hilo kwaTPL.
5. Mazingatio ya kibiashara
5.1 Mamlaka ya
kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania
Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL
inasingizia kwamba leseni ya matangazo
ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa
kuukubali "lock, stock and barrel."
5.2 TPL
inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na
Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship
agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa
miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo
wahusika wote ni lazima
wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa mfano,
moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni
yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii
itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA Dar es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni
shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika
mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato
takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa
kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata
siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa,
wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja
kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya Utendaji ya YANGA ina
maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde
maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television
hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake
urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo wa TPL kuwa lazima
Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya
Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu
michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha
YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
………………………………………..
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
Young Africans Sports Club
29 JULAI,
2013
No comments:
Post a Comment