UONGOZI wa timu ya soka ya Rhino Rangers ya Tabora umemteua Sebastian Nkoma kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kuchukua nafasi ya Renatus Shija aliyetimuliwa wiki iliyopita.
Akizungumza kwa njia ya simu leo, Katibu wa Rhino Rangers, Clarence Kambona alisema kuwa
wamemchukua Sebastian kwa kuwa ni kocha makini na mwenye mafanikio kwenye
ufundishaji wa soka.
“Kutokana na maazimio ya kikao kilichokaa baada ya kuondolewa
madarakani makocha wetu, uongozi ulimteua Sebastian kuifundisha timu yetu
ambayo kwa sasa iko katika maandalizi ya msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu,
na msaidizi wake atakuwa Emanuel Gift,” alisema Kambona.
Rhino iliwatupia virago makocha wake Renatus Shija na Hamadi
Mgongo waliopandisha daraja timu hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kutokuwa na viwango vya kufundishsa timu za Ligi Kuu.
Kocha mpya wa Rhino kwa mara ya mwisho alikuwa anafundisha
timu ya Jamhuri ya Pemba ambayo ili iliwakilisha nchi kwenye kombe la
Shirikisho barani Afrika.
No comments:
Post a Comment