KLABU ya Arsenal inaonekana kama imechemka, katika mbio za kumwania nyota wake wa zamani, Cesc Fabregas, baada ya kutangaza kuwa haitashindana tena na Manchester United katika mbio za kumfukuzia nyota huyo.
Kutokana na hali hiyo, inaelezwa
kuwa inaweza kushuhudiwa, Fabregas akirejea
England akiwa katika jezi za Manchester
United, baada ya kocha wa Gunners, Arsene Wenger kujiweka kando na kumuachia
mpinzani wake, David Moyes amnyakue nyota huyo wa Barcelona akifahamu kuwa
klabu yake itachukua nusu ya ada ya usajili wake.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star,
Manchester United imeshaweka mezani fungu la pauni milioni 26, kwa ajili ya
kumnasa kiungo huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Nou Camp, miaka miwili
iliyopita.
Arsenal ilisema jana kuwa kwa
kurejesha fungu la pauni milioni 25 pamoja na asilimia 50, itakuwa ni faida kwao, baada ya kumuuza Fabregas
kwa vinara hao wa Catalans kwa thamani ya pauni 30.
Wenger alisema jana kuwa hana tena
mpango wa kumfuatilia tena Fabregas na hivyo kuiachia njia Manchester United.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kwa
upande wake, Barcelona nayo inaonekana kutoikubali kutoka klabu hiyo ya Old Trafford, tangu ofa ya kwanza ya chaguo
la kwanza la Moyes, Thiago Alcantara kukataliwa.
Pia kwa mazingira hayo, imebaki
kushuhudiwa aidha kwa Fabregas, 26 akijiandaa kutua Manchester United akicheza
kwenye nafasi ya kati kama alivyokuwa Arsenal.
Inaelezwa pia kwamba, Fabregas ni mchezaji
ambaye amekuwa akiwindwa na kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson
tangu timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Old Trafford Oktoba 2004.
Kwa sasa Fabregas anasemekana kuwa
miongoni mwa nyota kadhaa ambao wapo mguu nje mguu ndani katika klabu ya Barcelona,
ambayo imetoa dau kubwa ili kumnasa nyota wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar
huku ikiwa na Lionel Messi.
No comments:
Post a Comment