Shahid Khan,
mmiliki mpya wa timu ya Fulham, akiteta
na mmiliki mwenzake wa timu ya NFL, Bob Kraft, kabla ya mtanange wa soka la Marekani uliofanyika hivi karibuni mjini Florida.
BILIONEA, Shahid Khan usiku
wa kuamkia juzi amekuwa tajiri mpya kuingia kwenye orodha ya mabilionea
wanaomiliki timu za michuano ya Ligi Kuu
ya England. Arsenal — Stan Kroenke, Marekani
Aston Villa — Randy Lerner, Marekani
Cardiff City — Vincent Tan, Malaysia
Chelsea — Roman Abramovich, Russia
Hull City — Assem Allam, Misri
Liverpool — John W Henry, Marekani
Manchester City — Sheikh Mansour, Abu Dhabi
Manchester United — Malcolm Glazer, Marekani
Sunderland — Ellis Short, Marekani
Hadi anaingia kwenye orodha hiyo, ilimlazimu Khan kujikamua kitita cha pauni milioni 150 ili kuchukua mikoba ya mmiliki wa zamani wa timu hiyo, Mohamed Fayed, ambaye ameamua kuiuza klabu hiyo ya Craven Cottage.
Mzaliwa huyo wa Pakistan, ambaye ni tajiri wa kuuza vipuri vya magari na mmoja kati ya vigogo wanaomiliki timu inayocheza Ligi ya NFL ya nchini Marekani, iitwayo Jacksonville Jaguars, atakuwa ameungana na vigogo tisa wanaomiliki timu katika ligi hiyo.
Ifuatayo ni orodha ya vigogo wengine wanaomiliki timu hizo ambao Khan, (62), atapambana nao katika kutafuta mafanikio ya soka nchini England, kama anavyofanya nchini Marekani.
Kama alivyo Khan, Kroenke ana jina katika medani ya soka nchini Marekani, kwani naye pia anamiliki timu kwenye michuano ya ligi ya NFL, iitwayo St Louis Rams.
Lerner (wa
kwanza kulia) akiangalia mazoezi ya timu yake ya Aston Villa.
Kabla ya kuinyakua timu hiyo, Lerner alikuwa miongoni mwa vigogo wanne waliokuwa
wakiwania klabu hiyo ya Aston Villa tangu Martin O’Neill aondolewe kwa maandamano mwaka 2010. Mzaliwa huyo wa jiji la New York, ambaye ni mmiliki wa zamani wa timu ya Cleveland Browns, ilimlazimu kujikamua pauni milioni 300 ili aweze kukamata usukani wa kuiongoza timu hiyo.
.
Mbali na kubadili rangi ya jezi, vilevile alibadili jina la kimichezo lililokuwa likitumiwa na klabu hiyo la Bluebirds na kuwa Red Dragons.
Hata hivvyo imani yake hiyo ilimlipa mwaka jana, baada ya klabu hiyo ya ligi ya nchini Wales kuweza kuleta ushindani mkubwa katika mbio za kuwania ubingwa.
Mashabiki wa
Chelsa wakimsalimia bilionea, Abramovich, baada ya kuinunua timu hiyo mwaka 2003.
Kwa ujumla Abramovich wakati alipoinunua timu hiyo kutoka mikononi mwa
mfanyabiashara, Kenneth William Bates miaka
kumi iliyopita, alionekana asingeweza kudumu nayo.Hata hivyo, baadaye aliiwezesha Chelsea kutwaa mataji mbalimbali, yakiwamo ya Ligi Kuu, licha ya kukaliwa kooni na mashabiki kwa sera yake zake za kutimua makocha.
.
Allam, (kushoto)
akitambulishwa na Mwenyekiti wake, Russell Bartlett (katikati) na mwanaye, Ehab,
baada ya kuinunua timu hiyo.
Allam alitua Hull City mwaka 2010, baada
ya klabu hiyo kukumbwa na ukata kutokana na kushuka daraja. Hata hivyo, mmiliki huyo wa viwanda ambaye aliondoka nchini kwao Misri mwaka 1968, alilazimika kutumia pauni milioni 36 kwa ajili ya kuimarisha safu ya uongozi ndani ya klabu hiyo ya Tigers na mwaka jana fedha hiyo ilimlipa, baada ya kurejea tena Ligi Kuu.
.
Henry (kulia)
na mkewe, Linda Pizzuti, wakishuhudia
moja ya mechi za timu hiyo.
Kama ilivyo kwa matajiri wengine, Henry ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Fenway Sports Group na pia ni tajiri ambaye anamiliki timu katika ligi mbili.
Mmiliki huyo wa Liverpool, vilevile ndiye kiongozi mkuu wa timu ya Boston Red Sox na aliweza kuichukua klabu hiyo ya Anfield kutoka mikononi mwa raia wengine wa Marekani, Tom Hicks na George Gillett, mwaka 2010.
Hata hivyo, naye alijikuta akiingia utata na mashabiki wa timu hiyo, baada ya Mei mwaka jana kumtimua aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Kenny Dalglish.
Sheikh
Mansour (wa pili kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwasalimia mashabiki wa
Manchester City siku ya kwanza alipowasili kwenye klabu hiyo ya Etihad.
Tajiri huyo kutoka familia ya kifalme nchi za Kiarabu, ameibadilisha mno klabu hiyo ya Ligi Kuu tangu alipoichukua kutoka mikononi mwa Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand, Thaksin Shinawatra.
Inaelezwa kwamba familia ya Mansour ina utajiri unaozidi wa Roman Abramovich mara sita na kwamba utajiri huo ndio ulioiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka jana na pia umeifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa timu zinazopigania ubingwa.
.
Mashabiki wa
Manchester United wakiandamana dhidi ya utawala wa Glazer mwaka 2010
Kibopa huyo raia wa Marekani aliichukua timu hiyo mwaka 2005 na ni mmoja wa wamiliki wenye mafanikio makubwa katika historia ya soka la England.
Hata hivyo, pamoja na kuandamwa na mashabiki, hasira hizo zilipungua mwaka jana alipoiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa 20 wa michuano ya Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Ellis akitabasamu
mbele ya mashabiki baada ya kuinunua timu hiyo.
Inaelezwa kuwa tajiri huyo ni kati ya matajiri ambao wanasaka mafanikio katika
medani ya soka kwa udi na uvumba. Hata hivyo umaarufu wa tajiri huyo raia wa Marekani unadaiwa kuongezeka zaidi baada ya kuinusuru Sunderland isishuke daraja mwaka huu.
No comments:
Post a Comment