LONDON, England
STRAIKA, Romelu Lukaku amesema kuwa anataka kuwa mchezaji mahiri Chelsea kama alivyokuwa, Didier Drogba.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, nyota huyo alisema juzi kuwa kwa urefu wake wa futi 6 na inchi 3, ndiyo anataka kuutumia kumsaidia kufanya hivyo kama alivyokuwa Drogba.
Katika mahojiano na gazeti hilo, Lukaku ambaye ameshapachikwa jina la Drogba mpya, alisema kuwa nyota huyo alishakuwa mahiri na kilichobaki ni juu yake kufanya kile alichokifanya raia huyo wa Ivory Coast: “Didier tayari ni mahiri. Sasa ni juu yangu kufanya kile alichofanya.
“Na ninataka kufikia mafanikio hayo haraka iwezekanavyo.”
Lukaku alisema ana uhakika wa kufanya hivyo kabla ya kufikia miaka 35.
Akijipa matumaini hayo zaidi, raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 20, alisema kuwa Drogba ni mmoja kati ya marafiki zake wakubwa na ndiye aliyemtengeneza umbo lake wakati akikipiga kwenye timu hiyo ya Chelsea.
“Baada ya mazoezi tulikuwa tukiongeza kwa saa nzima ama zaidi,” alisema Lukaku.
“Tuna uhusiano mzuri na bado tunazungumza kila siku. Na kila siku huwa namueleza kinachoendelea mazoezini na huwa ananieleza kama ni sahihi ama la.
No comments:
Post a Comment