KLABU ya Arsenal imepata pigo lingine baada ya beki wake wa kushoto Nacho Monreal kuingia katika orodha ya wachezaji majeruhi baada ya kuumia mgongo wakati akiwa katika mapumziko yake. Monreal mwenye umri wa miaka 27 alipewa mapumziko ya
ziada baada
kushiriki katika ya Kombe la Shirikisho akiwa na timu ya taifa ya Hispania hatua
iliyopelekea kukosa ziara ya kujiandaa na msimu mpya ya Arsenal nchini Japan.
Lakini akiwa mapumzikoni Monreal aliumia mgongo na Wenger hafamu chanzo cha
kuumia kwa beki huyo ambaye atakosa mechi za mwanzoni mwa msimu. Ukuta wa timu
ya Arsenal unaweza kuwa dhaifu mwanzoni mwa msimu 2013-2014 baada ya Thomas
Vermaelen, Laurent Koscielny na golikipa Wojciech Szczesny nao pia wakiwa
majeruhi.
No comments:
Post a Comment