RAIA wa Argentina, Gerardo Martino, Kocha wa Newell’s Old Boys ya huko Argentina, anatarajiwa kutangazwa kuwa Meneja mpya wa FC Barcelona kuchukua nafasi ya Tito Vilanova alieondoka kwa sababu za kiafya.
Martino, mwenye Miaka 50, anategemewa kusaini Mkataba wa Miaka mitatu na kutangazwa rasmi baadae Wiki hii.
Akiwa Nou Camp, Gerardo Martino atakuwa pamoja na Wasaidizi wake mwenyewe ambao ni Elvio Paolorrosso, Kocha wa Viungo, na Msaidizi Jorge Pautasso.
Martino, au ‘Tata’
kama alivyo maarufu, anakuwa Muargentina wa nne kuwa Kocha wa Barcelona wengine ni
Helenio Herrera, Roque Olsen na Cesar Luis Menotti na anatua Nuo Camp kuungana
na Supastaa wa Argentina Lionel Messi ambae amemsifia sana Kocha huyu.
Jumatano, Barcelona inacheza Mechi
ya Kirafiki na Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich na itakuwa chini Jordi Roura
kwenye Mechi hiyo iatakayochezwa huko Allianz Arena, Munich.
No comments:
Post a Comment